Forum Navigation
You need to log in to create posts and topics.

Chemsha bongo

Katika jamii zetu, inajulikana wazi kwamba wanaume huwa wanakula mara chache kwa siku, lakini milo hio huwa imejizatiti, lakini kwa vile kazi na shughuli za wanaume huwa ni ngumu na harakati zao ni nyingi kwahiyo ile milo huwa inatumika vizuri mwilini. Hatuna wasiwasi juu ya hilo.

Ukija upande wa pili, wanawake huwa wanakula kidogo ila wanakula mara kwa mara kushinda wanaume. Na wanawake huwa shughuli zao sio pevu kama za wanaume, jambo linalonifanya nijiulize juu ya matumizi ya wanga iliyopo kwenye chakula chao, na ukizingatia kuwa wengi hawafanyagi mazoezi na hata hawachezi. Isitoshe, wanawake ndio wanaongoza kula vyakula visivyo rasmi (junk foods) ambavyo tunajua sio salama sana kwa afya.

Kinachokuja kunishangaza ni kwamba licha ya yote haya, wanawake huwa wanafanikiwa kuishi maisha marefu zaidi kuliko wanaume. Wataalamu kuna yeyote anayeweza kunipatia ufumbuzi katika hili?

error: Content is protected !!