Usile hadi uhisi njaa ; usile baada ya kushiba :
Quote from aimlly on October 28, 2023, 5:13 amTunakula kwa ajili ya njaa, ila mara nyingi huwa si hivyo, unaweza ukajichunguza. Asilani ni muhim sana kula mpaka utakapohisi njaa. Ni njia bora ya kusimamia ulaji wako lakini pia, chakula kinaonekana kuwa na mvuto na ladha zaidi. Hilo halipingiki. Kula kwa ajili ya sababu zengine sio vibaya, lakini yaweza dhuru ikiwa ndio tabia. Hiyo inasababisha kula zaidi ya unachohitaji na hicho ni kichochezi cha ongezeko la uzito pamoja na madhara yake yanayofuata.
Tukigeuza shillingi, inashauriwa kuacha kula pale tu unapoanza kuhisi shibe na si zaidi ya hapo. Sababu ni hiyohiyo ya kuepusha kuzidisha viwango kuliko vinavyohitajika hasa kiwango cha wanga ambacho ndio huwa tunakula zaidi. Madhara mengine ya haraka ni kulevya na usingizi usiotarajiwa.
NITAWEZAJE ?
Njia mojawapo ni hii hapa. Ukiitazama sahani yako, pima asilimia 80 ya kile kiwango kinachotosha kukushibisha. Unaweza ukajiuliza kwanini? Sababu ni kuwa akili huchelewa kuitambua shibe kwa dakika takribani 20, kwahiyo mpaka unahisi shibe, tayari umeshakula kiwango zaidi. Hivyo basi tunapokula, nia iwe ni kuridhika na kuondoa njaa, sio kushiba. Na kula harakaharaka sana si vizuri kwani akili yako inahitaji walau dakika 20 kuitambua shibe, wakati huo wewe umeshaondoka mezani muda tu na inapelekea kula kiwango kingi zaidi kuliko unachostahili.
Mwili wako ni mwerevu, njaa ni kiashirio kwamba mwili unahitaji. Kula hadi unapohisi njaa na kuacha pale unapoanza tu kuhisi shibe ni njia bora cha kula kile kiwango ambacho mwili wako unahitaji.
Tunakula kwa ajili ya njaa, ila mara nyingi huwa si hivyo, unaweza ukajichunguza. Asilani ni muhim sana kula mpaka utakapohisi njaa. Ni njia bora ya kusimamia ulaji wako lakini pia, chakula kinaonekana kuwa na mvuto na ladha zaidi. Hilo halipingiki. Kula kwa ajili ya sababu zengine sio vibaya, lakini yaweza dhuru ikiwa ndio tabia. Hiyo inasababisha kula zaidi ya unachohitaji na hicho ni kichochezi cha ongezeko la uzito pamoja na madhara yake yanayofuata.