JINSI YA KUPANGA MLO KAMILI
Quote from Guest on April 15, 2024, 6:26 pmKula walau milo 3 iliyo kamili na ususa ( vitafunwa ) walau mara 2 kwa siku pamoja na kunywa maji ya kutosha kuanzia lita 1.5 chagua vyakula kutoka kila kundi katika makundi YAFUATAYO.
1. Vyakula vya nafaka, viazi, muhogo na ndizi
Kwa mfano: mahindi, mtama, mchele, ulezi, ngano, muhogo, ndizi za kupika, viazi vikuu na magimbi.
2. Vyakula vya jamii ya kunde na vya asili ya wanyama
Kwa mfano: maharage, njegere, karanga, mbaazi, kunde, nyama, mayai, maziwa, samaki, dagaa, kuku na wadudu wanaoliwa kama vile senene, kumbikumbi.
3. Matunda
Kwa mfano: embe, ndizi mbivu, papai, pera, chungwa, ubuyu, nanasi, pasheni, parachichi na zambarau.
4. Mbogamboga.
Kwa mfano: mchicha, majani ya maboga, kisamvu, matembele, bamia, karoti, nyanya chungu, nyanya, matango, mlenda, boga na biringanya.
5. Mafuta na sukari.
Kwa mafano: mafuta ya alizeti, nazi, mawese, mbegu zitoazo mafuta, majarini, siagi, sukari na asali.
NB: lishe bora hukusaidia kuwa na afya bora, kuzuia upingufu wa damu, kuboresha kuwaji wa kimwili na kiakili hasa kwa watoto. Kuutayarisha mwili kwa ajili ya kunyonyesha.
Kula walau milo 3 iliyo kamili na ususa ( vitafunwa ) walau mara 2 kwa siku pamoja na kunywa maji ya kutosha kuanzia lita 1.5 chagua vyakula kutoka kila kundi katika makundi YAFUATAYO.