Forum Navigation
You need to log in to create posts and topics.

Kwanini coca cola ni tamu sana ndani ya chupa ?

Kabla ya kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili sote tunatakiwa tujue kwamba production ya coke au coca cola soda yote inafanyika as one unit.

Hata mimi mara ya kwanza nilikua najiuliza kwanini ukinywa soda ya coca cola ambayo imekuwa packaged kwenye ile chupa ya glass (kitaalamu inaitwa RGB bottles) inakuwa na ladha nzuri na tamu zaidi kuliko ukinywa coca ambayo imekuwa packaged kwenye hizi chupa za plastiki..!

Nilikua nadhani huenda hizi soda mbili hutengenezwa tofauti kwahiyo huenda ikawa ni formulation za kwenye uchanganyaji lakin baada ya kufanya research nikagundua kuwa sio kweli na ukweli ni kwamba soda hizi zote zinaandaliwa kwa pamoja na baadae ndio wanaamua kuzihifadhi katika hizo packaging za RGB au za plastiki kulingana na ratiba ya order za siku husika.

Kwahiyo kwanini coka ya kwenye RGB ni tamu zaidi kuliko ya kwenye chupa za plastiki ?  

Chupa za plastiki kwa ujumla hua zinatengenezwa kwa kutumia material zinazoitwa PET au kwa kitaalamu zaidi Polyethylene Terephthalate , haya material yana sifa nzuri sana ambazo hufanya kupendwa kutumika katika kutengeneza chupa zinazotumika kubebea hizi soda. Baadhi ya sifa zake ni kama vile wepesi hivyo mteja hatoona uzito kubeba soda yake,zinaonyesha ndani hivyo mtu anaweza kuona vizuri kilichomo ndani ya chupa husika,hata hivyo pia material haya yanauwezo mzuri wa kuzuia gesi kutoka katika chupa husika.

Ukiachana na sifa hizi nzuri za hii material inayotumika kutengenezea chupa hizi za plastiki kuna madhaifu yake pia ila kwa hapa nitazungumzia madhaifu yanayoendana na swali letu; Katika utengenezaji wa hizi PET huwa kuna mabaki au kitaalamu tunaita by-products zake ambazo ni acetaldehyde ambayo ikichanganyikana na soda huwa inabadilisha ladha halisi ya soda lakini pia kuna catalyst ambazo hutumika katika utengenezaji wa hizi PET ambazo kitaalamu huitwa Antimony trioxide hizi pia zinaweza zikaleach ndani ya soda husika endapo soda hiyo haitohifadhiwa vizuri na kusababisha kubadilisha ladha ya soda hiyo.

Vilevile RGB au chupa za glass huwa zina sifa ya kutokuwa na uwezo wa kuchanganyika kikemikali na kitu kingine ( they are chemically inert) hivyo basi soda inayohifadhiwa humo huwa salama na haiwezi kubadilika ladha yake,na kupelekea soda iliyo ndani ya chupa ya RGB au chupa ya glasi kuwa tamu sana kuliko soda iliyo ndani ya chupa ya plastiki...

error: Content is protected !!