Quote from Omari Kitula on July 18, 2025, 8:32 amKatika dunia ya sasa ambapo bidhaa za chakula zimejaa madukani na sokoni, ni muhimu sana kwa mlaji kuwa makini kabla ya kufanya uamuzi wa kununua. Hapa kuna mambo matatu ya msingi ambayo kila mtumiaji wa chakula anapaswa kuzingatia ambayo hata mimi mwenyewe huwa siwezi kununua bidhaa yoyote ya chakula bila kuangalia hayo mambo. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo;
1. Angalia Tarehe ya Mwisho wa Matumizi (Expiry Date)
Usinunue bidhaa yoyote bila kuangalia tarehe yake ya mwisho wa matumizi. Bidhaa zilizokwisha muda wake zinaweza kusababisha madhara kiafya, hasa kwa watoto na wazee.
2. Soma Lebo ya Bidhaa
Lebo hukupa taarifa muhimu kuhusu:
》Viambato vilivyotumika
》Thamani ya virutubisho (nutritional value)
》Asili ya bidhaa (imezalishwa wapi)
》Maelekezo ya matumizi na uhifadhi
Kusoma lebo kunakusaidia kufanya maamuzi bora kwa afya yako.
3. Angalia Ubora na Ufungashaji
Bidhaa bora huja katika vifungashio safi, visivyoharibika, na vilivyofungwa vizuri. Epuka bidhaa zilizo na:
》Ufungashaji uliolegea au kuharibika
》Madoa, kutu, au harufu isiyo ya kawaida
》Bidhaa zisizo na jina la mtengenezaji au zenye maandishi yasiyoeleweka
Kuwa mlaji makini ni hatua ya kwanza ya kulinda afya yako na familia yako.
Katika dunia ya sasa ambapo bidhaa za chakula zimejaa madukani na sokoni, ni muhimu sana kwa mlaji kuwa makini kabla ya kufanya uamuzi wa kununua. Hapa kuna mambo matatu ya msingi ambayo kila mtumiaji wa chakula anapaswa kuzingatia ambayo hata mimi mwenyewe huwa siwezi kununua bidhaa yoyote ya chakula bila kuangalia hayo mambo. Mambo yenyewe ni kama yafuatayo;